Psalms 22:27-31


27 aMiisho yote ya dunia itakumbuka
na kumgeukia Bwana,
nazo jamaa zote za mataifa
watasujudu mbele zake,

28 bkwa maana ufalme ni wa Bwana
naye hutawala juu ya mataifa.


29 cMatajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu.
Wote waendao mavumbini
watapiga magoti mbele yake,
wote ambao hawawezi
kudumisha uhai wao.

30 dWazao wa baadaye watamtumikia yeye;
vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana.

31 eWatatangaza haki yake kwa watu
ambao hawajazaliwa bado,
kwa maana yeye ametenda hili.
Copyright information for SwhKC